Mwandishi
amesawiri suala la ndoa kupitia wahusika wafuatao:
¾
Yona na
Sara, Neema na Bunju na hata
Asna. Kupitia ndoa za wahusika hawa masuala mengi ya mahusiano katika ndoa
yanajadiliwa.
¾
Ndoa ya Yona
na Sara inasawiriwa kama ndoa ya kizazi cha jana.Inaonyesha matarajio ya ndoa
kulingana na jamii yao. Inaakisi malezi, majukumu ya mke na mume na matarajio ya
wanajamii kuhusiana na watoto. Inachora picha ya majukumu kama yalivyopangwa na jamii ya Yona
na Sara.
¾
Kulingana na
jamii katika tamthilia ya Bembea ya Maisha, mwanamke anapoolewa anahitajika
kuanzisha familia na mumewe. Anatarajiwa kujifungua watoto wa kike na vva
kiume. Katika ndoa ya Yona na Sara, tunafahamishwa kuwa wanajamii waliwasema
na kuwatafuna kama chingamu huku Yona akiitwa gumba na Sara kuitwa tasa. Hii ni baada ya
kuoana na kukaa kwa muda mrefu bila kujaliwa na watoto (uk. 6). Ni wazi kwamba ndoa ya Yona na Sara imenyimwa hadhi katika
jamii kwa kukosa mtoto wa kiume (uk. 7).
¾
Kulingana na
kizazi cha jana, mke anatarajiwa kujifungua watoto wa kike na wa kiume na hasa wale wa
kiume. Ndoa ya Yona na Sara inasutwa na kukejeliwa na wanajamii kwa kukosa
mtoto wa kiume ambaye aliaminika angekuwa mrithi wa Yona (uk. 8). Wanajamii
walimtaka Yona kumwoa mke ambaye angemzalia watoto wa kiume. Kulingana nao, Sara alikuwa
ameshindwa kumzalia mtoto wa kiume. Unyanyapaa huu ulimsukuma Yona kuupokea ulevi na kuanza kumpiga Sara kipigo cha mbwa kwa
kuwa hakumzalia mtoto wa kiume (uk. 9-10).
¾
Ni wazi
kwamba ndoa ya Yona na Sara imenyimwa nafasi na hadhi katika jamii kwa kukosa mtoto wa
kiume.
¾
Ndoa pia
imesawiriwa kama kitu chema ingawa chenye changamoto zinazoweza kuvumiliwa. Sara anasema
kuwa ndoa ni uvumilivu na wala Sio watoto na hakuna ndoa isiyokosa doa. Sara anaivumilia
ndoa yake na Yona. Anavumilia kuchapwa, kudharauliwa na kudhulumiwa. Sara anamvumilia mumewe hata baada ya dhiki hizo.
Fauka ya hayo yote, anamshauri Neema aivumilie ndoa yake na Bunju. Vilevile,
anamshauri Asna kumtafuta mume aolewe (uk. 33, 67).
¾
Ndoa huakisi suala la
malezi. Yona na Sara wanaonyesha malezi kwa kuwalea mabinti wao. Sara anawafurahia watoto wake na
kujitahidi kuwalea ipasavyo.
¾
Ndoa ya Neema na
Bunju ni ya kizazi cha leo. Neema na Bunju wamesoma, wamehitimu na wameajiriwa na kuanza familia yao.
Wanashirikiana katika masuala ya matumizi ya
pesa. Bunju anashughulikia majukumu ya familia yake na Neema. Amemruhusu
¾
Ndoa ya Neema na
Bunju ni ya kizazi cha leo. Neema na Bunju wamesoma, wamehitimu na wameajiriwa na kuanza familia yao.
Wanashirikiana katika masuala ya matumizi ya
pesa. Bunju anashughulikia majukumu ya familia yake na Neema. Amemruhusu Neema
kutumia mshahara wake kuwasaidia wazazi wake. Ndoa katika tamthilia hii imesawiriwa kama uhusiano unaofaa kuleta heshima
na uvumilivu. Bunju anamlalamikia Neema kwa
kukosa kujulishwa kuwa mama mkwe wake anarejea kijijini
bila yeye kujulishwa. Suala hili linamkera sana Bunju na kumuona Neema kama mke asiye na heshima (uk. 48).
¾
Neema anasisitiza kuwa
amempa mumewe heshima ya kutosha (uk. 49). Jambo la ndoa
limesawiri majukumu ya mke na mume. Katika ndoa ya
Bunju na Neema, mume ana majukumu ya kulipa karo, kulipa kodi ya nyumba na majukumu mengine. Jambo hili linaonyesha kuwa Bunju
ni mume aliyewajibika. Kwa upande mwingine, Neema ana jukumu
la kuwatunza wazazi wake.
¾
Katika ndoa ya Sara
na Yona, Yona anasawiriwa kuwa na jukumu la kuwasomesha wanawe. Hata baada ya Sara kwenda mjini
kwa ajili ya matibabu, Yona anachukua majukumu
nyumbani kama vile kushughulikia mifugo na kuondoa mtama shambani.
Katika mwisho wa tamthilia, Yona anamwahidi Sara kuwa
atayachukua majukumu yote kama mumewe na atamshughulikia katika kila hali. Yona pia anaonyeshwa kuwa na jukumu la
kumjuza Sara kuhusu mikutano ya vyama vya
kina mama.
¾
Ndoa pia imesawiriwa kama
jambo lililojaa bughudha. Kulingana na Asna, ndoa ina
mateso na imejaa masharti mengi. Asna anaona ndoa ya dadake Neema imejawa na matatizo yasiyoweza kuvumilika. Anasema
kuwa Bunju ni mchoyo na asiyetaka kumsaidia
mtu (uk. 33, 45). Asna vilevile anaiona ndoa ya wazazi wake kama iliyojawa na mateso.
¾
Anamweleza mamake kuwa
amedhoofishwa na mateso aliyoyapata katika ndoa yake
(uk. 53). Hali hii inamfanya Asna kusawiriwa kama msichana anayetaka kuyajenga maisha yake bila mume.